Meneja wa klabu ya Olympic Lyon ya Ufaransa Bruno Genesio amessema kikosi chake kitahitaji asilimia “150” kufanikisha mpango wa kuwafunga mabingwa wa soka nchini England Manchester City.
Olympic Lyon watakua wenyeji wa mchezo wa leo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya, huku mashabiki wengi wa Ufaransa wakitarajia kuona furaha inaendelea kubaki kwao, kufuatia timu hiyo kupata matokeo ya kushangaza kwenye mpambano wa mwezi Septemba katika uwanja wa Etihad.
Man City wamekua na muendelea mzuri wa kupata ushindi baada yakupoteza mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya Olympic Lyon, na wanaongoza msimao wa kundi F, kufuatia ushindi walioupata kwenye michezo mitatu mfululizo.
Genesio amesema: “Tunakwenda kupambana na timu yenye uwezo mkubwa kisoka zaidi yetu, lakini kama mlivyoona katika mchezo uliopita, matokeo yaliyopatikana yaliwashangaza mshabiki wengi duniani, tunahitaji kufanya hivyo tukiwa nyumbani, lakini tutahitaji asilimia “150” ili kufanikisha mpango huo.”
Olympic Lyon wanakwenda kwenye mpambano wa leo, wakiwa hawana uhakika wa kumtumia mshambuliaji wao kutoka Ufaransa Nabil Fekir, ambaye aliumia misuli ya paja wakati wa mchezo wa ligi dhidi ya St Etienne mwishoni mwa juma lililopita.
Kwa upande wa meneja wa Man City Pep Guardiola amesema wapo tayari kwa mpambano wa leso usiku, na anaimani kubwa vyombo vya habari huenda vikaandika taarifa tofauti na ilivyokua kwenye mchezo wa kwanza ambao walikubali kisago cha mabao mawili kwa moja.
“Soka ni mchezo wa maajabu sana, lilikutokea jana huenda likaendelea kutokea ama mabadiliko makubwa yakaonekana, sina uhakika vyombo vya habari vitatoka na habari gani baada ya mchezo wetu na Olympic Lyon, lakini tusubiri dakika 90 ziamue.” Alisema Guardiola.
Hata hivyo Man City itawakosa Bernardo Silva, Ilkay Gundogan na Gabriel Jesus ambao hawakusafiri na kikosi hadi Ufaransa, kufautia majeraha yanayowakabili.
Viungo Kevin De Bruyne, beki wa pembeni Benjamin Mendy (wanaendelea kuuguza majeraha ya goti) pamoja na Claudio Bravo (kisigino) nao ni miongoni mwa watakaoukosa mchezo wa leo.