Mwimbaji wa RnB, Bruno Mars jana aliwaacha na mshangao mashabiki wa muziki duniani baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika kipengele kizito zaidi cha tuzo za Grammy 2018 zilizofanyika wikendi hii jijini New York nchini Marekani, akinyakua tuzo ya albam bora ya mwaka na nyingine tano.
‘24K Magic’ ilipenya na kumpa ushindi huo mnono Bruno Mars, ikizipiku “Awaken, My Love!” ya Childish Gambino, 4:44 ya Jay-Z, DAMN, Kendrick Lamar na Melodrama ya Lorde.
Ingawa Jay Z ndiye aliyekuwa ametawala katika vipengele vya tuzo hizo mwaka huu, ni Bruno Mars na Kendrick Lamar ambao walionekana kung’ara zaidi kwenye majina ya washindi.
Bruno Mars alinyakua jumla ya tuzo sita kubwa na kuwa mshindi wa juu zaidi mwaka huu.
Albam ya Kendrick Lamar ‘DAMN’ ilifanikiwa kupenya kwenye kipengele cha albam bora za hip hop, ikiiweka kando albam ya Jay Z ‘4:44’ ambayo wengi waliipa nafasi pia.
Jay Z ambaye aliamua kutotumbuiza kwenye tuzo hizo licha ya kutengewa muda awali, alishindwa kunyakua tuzo yoyote kwenye vipengele nane alivyokuwa ametajwa.
- Video: Goodluck Gozbert afunguka anavyowapa dili kubwa wasanii chipukizi
- Gumzo: Diamond amtuliza Wema kifuani hadharani
Katika hatua nyingine, tuzo hizo zilikosolewa kwa kukosa usawa baada ya wasanii wa kike kuambulia tuzo 17 kati ya tuzo 86 zilizokuwepo.
Wasanii wengi wa kike walipanda jukwani wakiwa na mavazi meupe katika kuonesha kuunga mkono kampeni inayoendelea ya #Metoo inayolaani vitendo vya unyanyasaji wa kingono uliofanywa au unaofanywa na baadhi ya watu wenye majina makubwa kwenye tasnia ya burudani.
Hii ni sehemu ya orodha ya washindi:
Album of the year: Bruno Mars – 24K Magic
Record of the year: Bruno Mars – 24K Magic
Song of the year: Bruno Mars – That’s What I Like
Best new artist: Alessia Cara
Best pop album: Ed Sheeran – ÷ (Divide)
Best rock album: The War On Drugs – A Deeper Understanding
Best R&B album: Bruno Mars – 24k Magic
Best rap album: Kendrick Lamar – Damn
Bofya HAPA kuona orodha kamili