Mlinda mlango mahiri wa nchini Italia, Gianluigi Buffon ameonyesha wasiwasi kuelekea msimu mpya wa ligi ya nchini humo huku akikitazama kikosi cha klabu ya Juventus ambacho kitakua kikitetea ubingwa wa Sirie A.

Buffon, ambaye amekua kwenye klabu ya Juventus kwa zaidi ya miaka kumi, amesema msimu ujao utakua ni wa kipekee kutokana na muonekano uliopo hivi sasa huko Juventus Stadium.

Buffon, mwenye umri wa miaka 37, amesema msimu uliopita wakati wakitwaa ubingwa wa ligi ya nchini Italia (Scudetto) pamoja na kombe la Italia (Coppa Italia) kikosi chao kilikua na wachezaji kama Arturo Vidal, Carlos Tevez pamoja na Andrea Pirlo ambao kwa sasa hawapo baada ya kuondoka.

Amesema uwepo wa wachezaji hao ulichangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa mafanikio hayo, na sasa hawana budi kuangalia changamoto mpya ambayo itawakabili wakiwa na wachezaji waliojiunga na Juventus kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Wachezaji ambao watakuwa na jukumu la kusaidiana na wengine klabuni hapo baada ya kusajiliwa katika majira ya kiangazi ni Paulo Dybala, Mario Mandzukic na Sami Khedira.

Hata hivyo Gigi Buffon, amewataka wadau wa soka kumuelewa kwamba hana maana kikosi chao kimepoteza muelekeo baada ya kuondokewa na wachezaji waliokuwepo msimu uliopita, bali amezungumzia uhalisia uliokuwepo na mafanikio waliyoyapata.

Mlinda mlango huyo amesisitiza kuendelezwa kwa makali ya Juventus kwa msimu ujao wa ligi ya nchini Italia mabayo inatarajia kuanza kutimua vumbi lake mwishoni mwa juma hili ambapo The Bianconeri wataanzia nyumbani Juventus Stadium kwa kupambana na Udanise.

22 Wa Starts Kwenda Uturuki Jumapili
Ni Balaa La kulipiza Kisasi Ama Kuendeleza Uteja