Kiungo Mshambuliaji ‘Winga’ Bukayo Saka hatajiunga na kikosi cha England kwa ajili ya majukumu ya kimataifa, kwa mujibu wa kocha wa Arsenal, Mikel Arteta.
Saka alikosekana katika Ushindi wa bao 1-0 wa ‘Washika Bunduki’ hao dhidi ya Manchester City juzi Jumapili (Oktoba 08) kutokana na kusumbuliwa na tatizo la misuli ya paja katika mechi za hivi karibuni.
Kukosekana kwa Saka kulimaliza msururu wake wa kucheza mechi 87 mfululizo za Ligi Kuu na Arteta amesema sasa hatashiriki mechi zijazo za England dhidi ya Australia Ijumaa na Italia Oktoba 17.
Arteta amesema: “Hapana, hatafanikiwa. Hajafanya mazoezi hata mchezo mmoja. Hatapatikana kucheza soka kwa sasa.”
Winga huyo mwenye umri wa miaka 22, alichechemea wakati Arsenal ilipopoteza dhidi ya Lens Jumanne iliyopita, baada ya kutolewa pia katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Bournemnouth.
Kocha wa England, Gareth Southgate, Alhamisi alisema kwamba hatajiweka hatarini na Saka licha ya mechi dhidi ya Italia itakuwa muhimu ya kufuzu kwa michuano ya Euro.
Southgate alisema mapema: “Naweza tu kupitia kile Mikel (Arteta) amesema kuhusu mechi chache zilizopita.
“Tunawaangalia wachezaji kama vile nchi yoyote. Siku zote kuna umakini kwa wachezaji wetu kwa sababu wanacheza mpira na klabu zao.
“Wakati mataifa mengine yote yanawaita wachezaji wanaocheza Ligi Kuu na hakuna anayeangalia jinsi wanavyowatunza na jinsi wanavyowafundisha.
“Tunapokuwa na mazungumzo mazuri na klabu zote, nadhani wote watakubali kwamba labda tutatoa maoni bora kuliko kila taifa lingine.
“Wana imani na sisi kwamba tunafanya maamuzi ambayo ni sahihi kwa muda mrefu wakati wowote tunapoweza. Tuna mechi 10 tu kwa mwaka. Na kuna wakati Bukayo, kwa mfano, hatujacheza kila wakati.
“Lakini kuna michezo fulani muhimu ambapo ikiwa inawezekana kuwa na wachezaji wako bora, basi unataka kuwa nao.
“Kwa hiyo tuna jukumu hilo la kufuzu kwa nchi lakini nimekuwa mchezaji, sijawahi kuhatarisha afya ya mwili ya mchezaji. Na mimi pia.”