Johansen Buberwa, Bukoba – Kagera.
Baadhi ya Wakulima wa Mahindi Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, wameiomba Serikali kuwasaidia juu ya tatizo la Ngedere ambao wamekuwa tishio kwa kula mazao yao, ambayo ni tegemeo lao kwa chakula na kuwaingizia kipato.
Wakizungumza na Dar24 Media, Wakulima haowa kata tano za Manispaa ya Bukoba, wamesemakwa sasa wanashindwa kufanya shughuli nyingine na kubaki wakilinda mashamba yao, kutokana na kuhofia hasara.
Hata hivyo, Diwani wa Kata ya Bakoba, Shabani Rashid amesema tayari wameanza kuchukua hatua kwa kuitisha mikutano ya hadhara ili kuona namna ya kupambana na adha wanayoipata Wakulima kutokana na Wanyama hao.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Idara ya Maliasili na Mazingira, Mwesiga Kigoye amesema kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, tayari wameanza kuchukua hatua za kuwafukuza Wanyama hao katika maeneo ya Wananchi na kuanzia katika kata ya Kitendaguro na kata nyingine zinazosumbuliwa na Wanyama hoa zitafikiwa.