Mwenyekiti mstaafu wa jumuiya ya wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo amemtaka mbunge wa kuteuliwa, Humphrey Polepole amwache Rais Samia Suluhu Hassan atekeleze majukumu yake.

Amesema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari akimjibu Polepole kuhusu lawama alizotoa dhidi ya Samia ambaye ni mwenyekiti wa CCM.

Hata hivyo Bulembo amemuomba Mwenyekiti wa chama hichoPhilip Mangula kumhoji Polepole katika kamati ya maadili kama ambavyo ilifanyika kwa Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba.

“kama Polepole anataka kutoka atoke atuachie CCM maana ana wenzake wanaomshawishi kuanzisha chama chao, asitapetape na kuongea mambo ambayo hayaeleweki.”amesema Bulembo

Dewji kuchangia Bilion 2 ujenzi Mo Simba Arena
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba Disemba 13, 2021