Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Young Africans Hassan Bumbuli amesema baadhi ya wachezaji wa kigeni wa klabu hiyo waliokua wameitwa kwenye timu zao za taifa watajiunga na kikosi kesho Alhamisi (Aprili Mosi).

Kikosi cha Young Africans Young Africans kinaendelea na maandalizi ya michezo ya Ligi Kuu na kombe la Shirikisho (ASFC), chini ya kocha mzawa Juma Mwambusi.

Bumbuli amesema wachezaji hao wanatarajiwa kuanza kuwasili jijini Dar es salaam kesho Alhamis (Aprili Mosi), baada ya kumaliza majukumu ya kuzitumikia timu zao za taifa kwenye harakati za kusaka nafasi ya kushiriki fainali za Afrika (AFCON 2021).

Amesema wachezaji wazawa waliokua wameitwa kwenye timu ya taifa ya Tanzania *Taifa Stars* tayari wameshajiunga na wenzao kambini tangu juzi Jumatatu (Machi 29), baada ya kumaliza mchezo dhidi ya Libya uliochezwa Jumapili, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

”Wachezaji waliokuwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ walishawasili tangu siku ya Jumatatu, wakati Saido Ntibazonkiza (Burundi), Tomombe Mukoko (Dr Congo) na Haruna Niyonzima (Rwanda) wataanza kuwasili kesho ya Alhamisi”.

Young Africans itaendelea na michezo ya Ligi Kuu Aprili 10 dhidi ya KMC FC Aprili 10, ambapo itakuwa mwenyeji Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati, inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kufikisha alama 50, ikifuatiwa na Simba SC yenye alama 46, huku Azam FC wapo nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 44.

Mbunge wa viti maalum Chadema atoa angalizo mafunzo JKT
Tetesi: Adam Adam awindwa Libya