Bunge la Seneti la Marekani limeidhinisha muswada wa Sheria wa udhibiti wa silaha za moto kwa raia wa Nchi hiyo.

Warepublican kumi na watano walijunga na Wademocrat katika bunge la congress kuidhinisha hatua hiyo kwa kura 65 dhidi ya 33 zilizopinga na hii ikiwa ni sheria muhimu zaidi kuhusu silaha kuwahi kuidhinishwa kwa karibu miaka 30.

Uidhinishwaji huu unafuatia ghasia kubwa za ufyatuaji risasi zilizotokea katika soko kubwa lililopo   Buffalo, New York, na  katika shule ya msingi iliyopo Uvalde, Texas, iliyosababisha vifo vya watu 31.

Muswada huo utatakiwa kupitishwa katika Bunge la wawakilishi kabla Rais Joe Biden kuusaini kuwa sheria.

Licha ya kwamba ni muhimu, lakini mapendekezo  ya sheria hii yana mapungufu ya kile ambacho Wademocrat na wanaharakati wamekuwa wakikiomba.

Sheria mpya inajumuisha uchunguzi wa kina wa historia kwa wanunuzi wa silaha walio chini ya miaka 2 na dola bilioni 15 zitatolewa na serikali ya shirikisho kwa ajili ya kudhamini mpango wa afya ya akili na kuboresha usalama wa shule.   

Muswada huu pia unamaliza kile kinachoitwa “boyfriend loophole” kwa kuzuia mauzo ya bunduki kwa wale waliopatikana na hatia ya kuwanyanyasa wenza wao wa kimapenzi ambao hawajaolewa.  

 

Mtibwa Sugar yatangaza vita ya KUFA au KUPONA
Kifaru: Nilitabiri ubingwa Young Africans, Simba imekosea