Bunge la 11 lililomalizika hapo jana limewaweka matumbo joto watumishi Serikalini kwa kupitisha muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali.
Aidha, katika muswada huo ambao unaonekana kuwabana watumishi wa Serikali, unasema mfanyakazi yeyote atakayeshindwa kutimiza majukumu kwa makusudi au kwa uzembe atakatwa mshahara kwa muda wa miezi sita.
Akiwasilisha maelezo ya muswada huo bungeni mjini Dodoma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesema katika kifungu cha 65(2) cha sheria ya bajeti kimeweka wazi masharti, ofisa yeyote akishindwa kutekeleza majukumu yake atakuwa ametenda kosa kinidhamu.
-
Video: Majaliwa ataka Baraza la Michezo Tanzania lichunguzwe, ampa agizo Mwakyembe
-
Video: Chadema wanena mazito kuhusu kamata kamata ndani ya chama
Hata hivyo, msemaji wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Hamidu Bobali amesema kuwa makato hayo ya mshahara kwa mfanyakazi kwa muda wa miezi sita bila kuzingatia hasara anayoweza kuisababishia Serikali itakuwa haina maana yeyote.