Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai, amewataka wabunge wateule wote kufika jijini Dodoma kwaajili ya usajili na taratibu zingine za kiutawala kwa ajili ya kikao cha kwanza cha bunge ambacho kitaanza novemba 10 hadi novemba 13 ambapo bunge litaahirishwa.

Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari, amesema shughuli ambazo zinatakiwa kufanyika katika mkutano huo ni kusoma tangazo la Rais la kuitisha Bunge na kwamba shughuli kubwa itakayo fanyika ni kumchagua spika wa bunge.

” Naomba niwafahamishe wabunge wote shughuli za usajili na taratibu nyingine za kiutawala zitafanyika bungeni Dodoma kuanzia novemba 7 hadi novemba 9 mwaka huu” amesema Kagaigai.

Aidha amesema kuwa baada ya spika wa bunge kuchaguliwa na kuapa kitakachofuaata ni kiapo cha wabunge wote wateule.

Amesema kuwa bunge litafanya shughuli nyingine ya kuthibitisha jina la Waziri Mkuu litakalokuwa limewasilishwa bungei na Rais John Magufuli.

Ahadi ya Joe Biden kwa wamarekani
Biden amburuza Trump uchaguzi mkuu Marekani