Bunge la Iran limeukataa utetezi wa Rais wa nchi hiyo, Hassan Rouhani walipomtaka ajieleze juu ya kuporomoka kwa uchumi na kupanda kwa gharama za maisha na limemtaka ajieleze mbele ya mahakama.
Rouhani ameliambia bunge hilo kuwa Iran itapambana na vikwazo ilivyowekewa tena na Marekani na kuapa kwamba serikali yake itaishinda njama yoyote iliyopangwa na nchi za Magharibi dhidi ya nchi hiyo.
Aidha, Bunge la Iran limemwita Rouhani kwa mara ya kwanza tangu alipoingia madarakani mwaka 2013, kujibu maswali juu ya kuzorota kwa uchumi na kuongezeka kwa ukosefu wa ajira.
“Hatutaruhusu kikundi cha wapinzani wa Iran ambacho leo kimekusanyika katika Ikulu ya Marekani kupanga njama dhidi yetu. White House haitakuwa na furaha kitakapomalizika kikao cha leo,” amesema Hassan Rouhani
Hata hivyo, katika hali isiyo ya kawaida, bunge lilipiga kura ya kutokuridhika na utetezi wa rais huyo mwenye msimamo wa wastani, wakisema kuwa katika masuala matano waliyomuuliza ni moja tu ndilo alilowatosheleza kwa maelezo.
-
Papa Francis awasili Ireland kwa masikitiko
-
Marekani yatuma Manowari ya kivita kuidhibiti Urusi na China
-
Marekani yapata pigo kubwa