Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeitaka serikali kutoa maelezo ya kina kuhusu watumishi wa Wizara ya Uvuvi na Mifugo kuvamia Mgahawa wa Bunge na kisha kuwapima samaki waliokuwa wakiuzwa, kitu ambacho kinadaiwa haikuwa sahihi.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson baada ya wabunge kuomba muongozo wa kiti ili suala hilo lijadiliwe bungeni.
Akiomba muongozo wa spika, mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba kwa kutumia kanuni ya 47 ya kutaka bunge lisimamishe shughuli zake ili kujadili jambo hilo.
Serukamba amesema kuwa maofisa uvuvi walivamia Mgahawa wa Bunge bila kutoa taarifa kwa Katibu wa Bunge, Spika wa Bunge wala Naibu Spika wa Bunge.
Aidha, maofisa hao waliingia jikoni bila kufuata utaratibu wowote na kuvaa vifaa mikononi na kuanza kupekua chakula ambacho tayari kilishapikwa, jambo ambalo linatishia usalama wa wabunge.
-
Mbuga tatu za wanyama Tanzania zatajwa kuwa bora zaidi Afrika 2018
-
Sekretarieti ya Maadili yawaweka mtegoni Wabunge
-
Majaliwa atoa agizo kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya
Hata hivyo, kutokana na hoja hiyo Naibu Spika wa Buge Dkt. Tulia Ackson alikuabaliana na hoja ya mbunge huyo na kutoa muda wa dakika 30 kujadili jambo hilo.