Rais wa Brazil, Dilma Rousseff ameondolewa madarakani na ‘Seneti’ kufuatia tuhuma za muda mrefu dhidi yake za kuchakachua bajeti ya nchi hiyo.

Rais huyo ameng’olewa baada ya wajumbe 61 kumpigia kura ya kutaka aondolewe dhidi ya kura 20 pekee zilizomtetea abaki kwenye nafasi hiyo.

Uamuzi huo wa kihistoria nchini humo umefikisha ukingoni utawala wa miaka 13 wa rais huyo mwanamama aliyekuwa shupavu kwenye masuala ya kisiasa na utawala wake.

Bunge hilo la Seneti limempitisha Michel Temer ambaye ameapishwa kushika nafasi ya Urais wa mpito kumalizia muhula wa Rousseff hadi Januari 1 Mwaka 2019.

Rais Michel Temer

Rais mpya wa Brazil, Michel Temer

Hata hivyo, Rousseff ameendelea kukanusha kwa nguvu zote tuhuma dhidi yake akidai ni hujuma na njama za kutaka kumuondoa madarakani.

 

The Three Lions Yapata Mtihani, Foster Aondoka Kambini
Klabu Za England Zavunja Rekodi Za Usajili, Pauni Bilioni Moja Yatumika