Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo juni 22, 2021 limepitisha bajeti ya makadirio na mapato ya Serikali nzima kwa mwaka wa fedha 2021/ 2022, ambapo kwa mara ya kwanza katika upigaji kura hauna kura ya Hapana.

Spika wa Bunge Job Ndugai ametangaza matokeo ya kura zilizopigwa na jumla ya wabunge 385 kati yao 23 hawakuamua sawa na asilimia 6, na walioamua ni 361 sawa na asilimia 94 ya kura hizo na 5 hawakufika bungeni.

Aidha Spika Ndugai amesema kuwa asilimia 94 iliyojitokeza katika bunge hili ni asilimia amabyo haijawai kutokea katika bunge kwa muda mrefu

Amesema kuwa bunge likikataa Bajeti inamaanisha halin imani na serikali, lakini kwa Bunge kupisha Bajeti hiyo kwa asilimia kubwa inamaana Bunge linaimani kubwa na serikali.

Halikadhilika Spika Ndugai ameipongeza serikali yote kwa ujumla kuanzia Rais Samia, lakini pia amewapongeza wabunge wote, kamati zote za hususani kamati ya bajeti.

Aidha Muswada wa sheria ya Serikali imehidhinisha Jumla ya Trillioni 36, Bilioni 681, Milioni 897 na laki 765000 kwa matumizi ya serikali kutoka katika mfuko mkuu wa hazina kwa mwaka unaoishia Tarehe Juni 30, 2022.

Morrison kukutana na Michael Filbert
Mabadiliko ya vitambulisho vya wajasiriamali