Bunge limepitisha kwa kauli moja, azimio la kuitwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti ili kuhojiwa na Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge.
Azimio hilo limetokana na hoja iliyowasilishwa na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara akisema wateule hao wa Rais wametoa kauli zinazodhalilisha hadhi ya mhimili huo wa Dola.
Akijibu swali kuhusu tuhuma dhidi yake zilizoibuliwa na wabunge kuhusu chanzo cha mali zake, Makonda amewaambia waandishi wa habari kuwa wakati mwingine watunga sheria hao hulala bungeni kwa kukosa cha kuzungumza.
Aidha, kutokana na wabunge kukerwa na kauli ya Makonda, mbunge wa Mkuranga (CCM), Abdallah Ulega ameomba mwongozo kuhusu suala hilo.
Hata hivyo, Mkuu wa wilaya, Mnyeti anadaiwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa wabunge ni wapuuzi kutokana na michango yao wakati walipohoji hatua ya Ma-DC na Ma-RC kutoa amri za kuwaweka mahabusu viongozi wa kisiasa