Mbunge Francis Mtega ni mmoja kati ya Wabunge ambaye alikuwa na jitihada za kuwatumikia wananchi wake wa jimbo lake la Mbarali na hata katika sekta ya afya kiujumla.

Mbunge huyu ameaga dunia Julai Mosi, 2023 majira ya asubuhi huko Chimala, Mbarali na kuacha vilio na simanzi kwa wana Mbarali, Taifa na wana medani za siasa kiujumla.

Francis Mtega. Pumzika kwa amani.

Wengi wamemlilia Mtega akiwemo Kiongozi wa nchi, Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ametuma Salaam za pole kwa Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, Wabunge, ndugu, jamaa na marafiki na wananchi wa Mbarali.

Rais samia katika Salam zake za pole anasema, “nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Mbunge wa Mbarali, Mheshimiwa Francis Mtega Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema. Amina.”

Wanasayansi wagundua shimo kubwa Baharini
Che Fondoh Malone kimeeleweka Simba SC