Msanii wa Nigeria, Burna Boy ameponda mfumo wa muziki wa Nigeria pamoja na tuzo zinazotolewa nchini humo akidai kuwa zimejaa ‘siasa’.

Akiongea na Jarida la The Fader, Burna Boy alisema kuwa hadhani kama yeye ni sehemu ya muziki wa Nigeria kwa sababu kiwanda cha muziki nchini humo kinaendeshwa na watu fulani kisiasa hali inayomfanya kukosa tuzo anazostahili.

Alieleza kuwa yeye amejiweka kando na siasa zinazoendelea kwenye kiwanda cha muziki huo na kujikita katika kufanya ngoma kali tu zinazompa mashabiki wengi licha ya kutokuwa na wafuasi wengi Instagram na Twitter kama wengine.

“Sina wafuasi wengi kihivyo kwenye Twitter au namba kubwa kwenye Instagram. Lakini nafanya vitu ambavyo watu wenye wafuasi milioni moja hawawezi kufanya,” alisema Burna boy.

Uturuki Yaigomea Tena Urusi
Picha: Wafungwa Wanawake washiriki shindano la Urimbwende ‘Miss Criminal’