Serikali ya Burundi imetangaza wiki moja ya maombolezo kutokana na kifo cha Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza.
Kifo cha Rais huyo kimetokea siku chache kabla ya rais mteule kutoka chama tawala cha CNDD-FDD Evariste Ndayishimiye kuapishwa baada ya kushinda uchaguzi wa mwezi Mei.
Hata hivyo viongozi wa mataifa mbali mbali wametoa salaam zao za rambi rambi kutokana na kifo cha Nkurunziza, Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, Paul Kagame wa Rwanda , Macky Sall wa Senegal ni miongoni mwa marais waliotoa salamu hizo.
Haifahamiki mara moja ni hatua gani serikali itachukua baada ya kifo cha rais huyo, Kwa mujibu wa katiba ya Burundi, rais anapofariki akiwa madarakani kabla hajakabidhi madaraka kwa rais mwingine, spika wa bunge anachukua madaraka na kutayarisha uchaguzi mwingine.