Tume ya uchaguzi nchini Burundi inatarajiwa kutangaza matokeo ya awali ya uchaguzi wa Urais uliofanyika Jumatano iliyopita.
Tume hiyo imewaambia waandishi wa habari kuwa itatangaza matokeo ya awali saa nane mchana majira ya Burundi, na matokeo kamili yatatangazwa Juni 4, 2020.
Matokeo ya muda yaliyochapishwa na Shirika la Habari la Taifa yamemuonyesha Evariste Ndayishimiye akiongoza kwa asilimia 80 ya kura zilizohesabiwa huku mpinzani wake mkuu, Agathon Rwasa akipata takriban asilimia 20.
Aidha, wagombea wengine 5 kwa pamoja wamepata asimilia moja ya kura zilizohesabiwa.
Msemaji wa Rwasa amesema kilichotokea ni mpango uliosukwa vyema na chama tawala wa kung’ang’ania madarakani.