Serikali ya Burundi imezipinga vikali takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi-UNHCR kuwa kuna wakimbizi zaidi ya 430,000 wanaohitaji misaada mwaka huu.
Nchio hiyo Imefikia hatua hiyo mara baada ya shirika hilo kuanza kampeni ya kuchangisha fedha zaidi ya dola milioni 300 kwa ajili ya kuwahudumia wakimbizi hao ambao asilimia 80 wanaishi katika kambi za wakimbizi nchi jirani.
Aidha, Burundi imesema kuwa UNCHR imekuwa ikidanganya juu ya idadi ya wakimbizi kutoka nchini humo ili iweze kujipatia kiwango kikubwa cha misaada kutoka kwa wafadhili.
Hata hivyo, Burundi imelituhumu shirika hilo kuwa linatumia mwanya huo kama njia ya kujipatia kipato, lakini uhalisia ni kwamba hakuna idadi kubwa ya wakimbizi kama hao.
-
Kesi ya Aveva, Kaburu yaahirishwa tena
-
Mzee Ruhsa mgeni rasmi Simba v Genarmarie
- Video: Wauza dawa za kulevya wawekwa kikaangoni