Mshambuliaji wa mabingwa wa soka Tanzania bara Dar es salaam young Africans, Malimi Busungu, amemtaka kocha wa, Hans van Der Pluijm kumpa angalau dakika 30 kwenye mchezo wa kesho Jumamosi wa Ligi Kuu Bara ili aivuruge Simba.

Busungu, straika aliyetua akitokea Mgambo ya Tanga, mwanzoni mwa msimu huu, amejikuta akiwa chaguo la tatu la Pluijm nyuma ya Amissi Tambwe na Donald Ngoma, alifikia hatua hiyo baada ya kudai kuwa ana bahati ya kuifunga Simba kila anapokutana nayo.

Busungu amesema tangu alipoanza kukutana na Simba, amekuwa akiifunga, hivyo anaamini endapo Pluijm atakubali ombi lake hilo la kumpatia dakika 30 kwenye mchezo huo, basi atawavuruga vibaya Simba kwa kuzifumania nyavu zao kwa zaidi ya mara moja.

“Najiamini kuwa naweza kufanya hivyo endapo nitapewa nafasi kwani ukuta wa Simba jinsi ulivyo hakika hakuna beki wa kunisumbua nisifanye yangu,” alisema Busungu.

Roberto Firmino Aondolewa Kikosini
CCM, Ukawa Wairuka MCT Kuhusu Mdahalo