Waziri wa Nishati Januari Makamba amesema serikali ya awamu ya sita katika kipindi cha mwaka mmja cha Rais Samia Suluhu Hassan imeonesha kasi kubwa katika kutekeleza miradi ya kimkakati ukiwemo wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP).

Amesema katika kipindi hicho Rais Samia ameidhinisha na kulipa kiasi cha sh.Trilioni 1.4 ikilinganiswa na sh. Trilioni 2 amabzo zililipwa kipindi cha serikali ya awamu ya tano chini ya Hayati John Pombe Magufuli na sasa mradi umefikia asilimia 56.

Waziri Makamba amesema hayo wakati wa ziara ya kamati ya kudumu ya bunge ya Nishati na Madini iliyotembelea meadi huo kwa lengo la kujiletea maendeleo.

Waziri wa Nishati, Januari Makamba ameiambia kamati ya bunge ya nishati na madini kwamba kasi ya utekelezaji mradi huo imeongezeka kutokana na mikakati kadhaa inayotekelezwa na serikali ikiwemo kumlipa mkandarasi kwa wakati.

Mradi huo wa megawati 2,115 ulianza wakati wa uongozi wa Hayati Rais John Magufuli ambaye (katika kipindi chake) aliidhinisha malipo ya Sh trilioni 2.

‘’Wabunge wa kamati hii wameridhishwa na kufurahia hatua iliyofikia, wamepongeza serikali , wizara na Tanesco na Rais kwa uwezeshaji wake na idhini yake ya kutoa malipo kwa wakati’’ amesema Makamba.

Pamoja na hayo amesema kasi hiyo ya mradi imetokana na mabadiliko ya uongozi na uendeshaji katika mradi huo ili kuhakikisha ubora na viwango vinafikiwa.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya Nishati na madini Dustani Kitadulu amesema kamati hiyo imeridhishwa na utekelezaji wa mradi huo kwa sasa ambapo kunatofauti kubwa na awali walipotembelea mradi huo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Maharage Chande amesema zipo changamoto chache amabazo zimefanya mradi huo kuchelewa ikiwemo ya ugonjwa wa Covid 19 ambapo ilisababisha ucheleweshwaji wa baadhi ya vifaa kutoka nje na kwasasa wanafanya tathmin ya mda gani utaongezeka katika mradi huo.

Ahadi ya Rais Samia Chato
Ismail Rage: Sikumaanisha hivyo