Wakulima na wafugaji katika maeneo ya Rufiji walikuwa wakiathiriwa na mafuriko ya maji ya mto Rufiji kwa miaka mingi, jambo ambalo liliathiri kaya nyingi.
Kuanza kufanya kazi kwa Bwawa la Nyerere kutasaidia kuondoa kadhia hiyo kwani maji yatapita kwa kiwango cha kutosha na kinachodhibitiwa.
Aidha, Bwawa hilo poa litaruhusu maji kiasi cha lita 200,000 kwa sekunde kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo yale ya kibinadamu.