Shirikisho la soka Barani Afrika ‘CAF’ linasubiri Oktoba 06 ili kukamilisha mpango wa kupanga makundi ya Michuano ya ngazi ya vilabu iliyo chini ya shirikisho hilo kwa msimu huu 2023/24.

CAF imewalazimu kusubiri hadi Oktoba 06, ili kutoa nafasi kwa mchezo mmoja wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hatua ya Mtoano ambao ulichezwa jana Jumatatu (Oktoba 02) kati ya Mabingwa wa Soka nchini Algeria Chabab Riadhi de Belouizdad (CR Belouizdad)  dhidi ya Bo Rangers ya Sierra Leone.

Mchezo wa mkondo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo mjini Bo nchini Sierra Leone, Chabab Riadhi de Belouizdad ilichomoza na ushindi wa mabao 3-1, na matokeo ya mchezo wa Mkondo wa Pili Chabab Riadhi de Belouizdad imechomoza na ushindi wa mabao 3-1 na kufuzu kwa jumla ya mabao 6-2.

Kwa matokeo hayo rasmi timu 16 zilizofuzu hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa zimefahamika na kuthibitishwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Pia Shirikisho hilo limethibitisha timu 16 zilizotinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika, ambapo pia Droo yake itachezeshwa Oktoba 06 mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

Timu 16 zimethibitishwa kuingia katika hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika hadi sasa, na tayari zimewekwa katika vyungu ama Pots, kusubiri Droo siku tatu zijazo.

Chungu cha Kwanza – Pot One

Al Ahly – Misri (83 pts)

Wydad AC – Morocco (74 pts)

Espérance de Tunis – Tunisia (56 pts)

Mamelodi Sundowns – Afrika Kusini (51 pts)

Chungu cha pili – Pot Two

CR Belouizdad – Algeria (36 pts)

Pyramids – Misri (35 pts)

Simba SC –  Tanzania (35 pts)

Petro de Luanda – Angola (33.5 pts)

Chungu cha Tatu – Pot Three

TP Mazembe – DR Congo (30.5 pts)

Al Hilal – Sudan (23 pts)

ASEC Mimosas – Ivory Coast (20 pts)

Young Africans – Tanzania (20 pts)

Chungu cha nne – Pot Four

Étoile du Sahel – Tunisia (20 pts)

Jwaneng Galaxy – Botswana (4 pts)

FC Nouadhibou – Mauritania (1 pt)

Medeama – Ghana

Jambo la muhimu katika upangaji wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ni kwamba timu zilizopo katika Chungu kimoja hazitapangwa kundi moja, bali kila timu kutoka kila chungu itakutana na timu nyingine kutoka kila chungu kutengeneza makundi manne tofauti.

Upande wa Kombe la Shirikisho klabu 16 zilizofanikiwa kutinga hatua ya makundi na kuthibitishwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika msimu huu 2023/24 nazo zimewekwa katika vyungu (Pots) vitatu tofauti.

Chungu cha Kwanza – Pot One

Zamalek – Misri (39 pts)

RS Berkane – Morocco (37 pts)

USM Alger – Algeria (27 pts)

Rivers United – Nigeria (10 pts)

Chungu cha Pili – Pot Two

Diables Noirs – Congo Brazzaville  (5 pts)

Sagrada Esperança – Angola (4 pts)

Future – Misri (2.5 pts)

Club Africain – Tunisia (2 pts)

Chungu cha Tatu – Pot 3

Académica do Lobito – Angola

Dreams FC – Ghana

Académie SOAR – Guinea

Abu Salim – Libya

Al Hilal Benghazi – Libya

Stade Malien – Mali

Sekhukhune United – Afrika Kusini

SuperSport United – Afrika Kusini

Jambo la muhimu katika upangaji wa makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika ni kwamba timu zilizopo katika Chungu kimoja hazitapangwa kundi moja, bali kila timu kutoka kila chungu itakutana na timu nyingine kutoka kila chungu kutengeneza makundi manne tofauti.

Agizo la Biteko: Aweso afika Ngara, aahidi uhakika wa Maji
Ongezeko la mshahara lasababisha mgomo wa Wafanyakazi