Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) limethibitisha kuwa Uwanja wa kimataifa wa Cairo utatumika kwa ajili ya mchezo wa fainali ya klabu bingwa Afrika kati ya Al Ahly dhidi ya Zamalek zote za Misri.

Katika pambano hilo mashabiki hawataruhusiwa kuhudhuria fainali hiyo ikiwa ni muendelezo wa mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Uwanja wa kimataifa wa Cairo

Aidha waandishi wa habari na viongozi takribani 2000 wataruhusiwa kuingia ndani ya dimba la Cairo International kushuhudia pambano hilo huku tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona zikizingatiwa.

Mchezo wa fainali Ligi ya Mabingwa Afrika umepangwa kuchezwa Novemba 27.

Rais Magufuli afanya uteuzi,amrudisha Mwakyembe
Viongozi BAVICHA wafutiwa mashtaka