Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ limetangaza maamuzi ya michezo miwili ya Kombe la Shirikisho kati ya CD 1 Agosto ya Angola na Namungo FC ya Tanzania, ambayo rasmi itachezwa nchini Tanzania.

Maamuzi hayo yamefanywa baada ya Kamati ya Mashindano ya CAF kubaini kuwa si Agosto wala Namungo iliyohusika moja kwa moja kukwamisha mchezo wa mkondo wa kwanza uliokuwa uchezwe Februari 14 mjini Luanda nchini Angola.

Michezo yote miwili inatakiwa kuchezwa angalau ndani ya saa 72, na iwe imechezwa kufikia Februari 26 mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba, CD 1 Agosto itakuwa mwenyeji wa mchezo wa kwanza, hivyo itawajibika katika maandalizi yote ikiwemo gharama za maofisa wa mchezo huo.

Kwa vile makundi ya Kombe la Shirikisho yatapangwa Februari 22, mshindi wa jumla baada ya michezo hiyo miwili atazingatiwa katika viwango (non-ranked) wakati wa upangaji.

Simba SC yatinga Musoma, Mara
Tanzia: Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif afariki dunia, Rais Magufuli amlilia