Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ limepanga kuja na muongozo mpya wa usimamiaji wa vipimo vya ugonjwa wa Corona *Covid-19* kutokana na changamoto nyingi zilizoibuka katikia mashindano yake mbalimbali inayoyasimamia.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya CAF, Alexander Siewe imesema kuwa shirikisho hilo linaandaa utaratibu mpya wa vipimo vya Covid-19 siku za usoni ili kuepusha migongano na malalamiko mengi kama ilivyotokea katika mashindano yake tofauti msimu huu.

“Kwa changamoto zilizoibuliwa kuhusiana na Covid-19 na vipimo vya PCR vinavyohitajika kwenye mashindano, mjadala umefikia makubaliano ya kutengeneza ushirikiano kwa kushirikiana na WHO (Shirika la Afya Duniani) na vyombo huru katika ufanyaji vipimo kabla ya mechi na hii itahusisha pia Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) Cameroon,” imesema taarifa hiyo.

Rais Samia awataka watendaji kuwajibika, "Ukinizingua tutazinguana"
Young Africans yamvutia kasi Nado