Imethibitika kuwa Tanzania itawakilishwa na timu mbili kwenye michuano ya kimataifa msimu wa 2020/21, baada ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kitendawili kilichokua kimekosa jibu kwa muda mrefu.

Simba SC itaiwakilisha nchi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kama mabingwa wa Tanzania Bara, na Namungo FC watashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kama washindi wa pili wa Kombe la Shirikisho (ASFC).

Young Africans na Azam FC ziliweka matumaini ya kushiriki michuano hiyo baada ya Libya kuahirisha ligi yao na Tanzania iliyokuwa na alama 14 ilikuwa na nafasi ya kupenya endapo Libya wangepigwa chini na CAF.

Taarifa rasmi iliyotolewa na CAF Septemba Mosi, 2020 imezitaja nchi  12 zenye pointi nyingi ambazo zitatoa timu nne kwenye michuano ya Bara la Afrika ikiwemo Libya ambayo haikumaliza msimu wake wa Ligi Kuu 2019/20.

Taarifa ya CAF imeeleza kuwa, nchi ambazo hazikumaliza ligi na zilitoa taarifa awali zinaruhusiwa kushiriki kwa mujibu wa msimamo wa Ligi wa nchi husika na alama.

Pia imeeleza kwa nchi ambazo ziliahirisha ligi zao, timu zitaendelea na uwakilishi kwenye michuano hiyo kulinga na uwiano utaotolewa na shirikisho la nchi husika.

CAF wamesema kwa nchi ambazo hazijamaliza ligi zao wana haki ya kuchagua njia mbili walizoainisha kabla ya kufungwa kwa dirisha.

Usajili wa timu hizo kwa nchi wanachama ulianza jana Septemba Mosi hadi Oktoba 20 na kutokana na janga la Corona Ligi nyingi zilisimama na nyingine kulazimisha kusimama CAF wametoa ufafanuzi suala hilo.

Ratiba ya mtoano itaanza kwa raundi ya kwanza Novemba 20-22 na kurudiana Novemba 27-29 huku hatua ya ya kwanza ikianza Desemba 11-13 na kurudiana 18-20.

Mliokosa vigezo kidato cha tano ombeni nafasi vyuo vya kati - Jafo
Macron awashukia viongozi Lebanon