Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) imebainisha kuwa Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro zilifadhili Tamasha la Upandaji Mlima Kilimanjaro  bila kuwepo kwenye bajeti.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, amesema shindano la ‘Kigwangalla Kili Challenge’ la mwaka 2019 lilitumia Milioni 172 zilizotolewa na TANAPA na Ngorongoro.

Ameongeza kuwa Waziri kupitia Kaimu Katibu wake alielekeza Mamlaka hizo kufadhili shindano.

Pia, CAG amesema Kaimu Katibu Wizara ya Utalii aliagiza Mamlaka ya Ngorongoro na Wakala wa Misitu (TFS) kulipia matumizi ya Ofisi ya Waziri ambapo Ngorongoro walitoa Milioni 92 na TFS Milioni 55.95.

Aidha ripoti hiyo imebainisha kutolewa kwa Tsh. Milioni 140 na Wizara ya Maliasili na Utalii ili kuilipa Kampuni ya Wasafi bila kusainiwa mkataba wowote.

CAG amesema Fedha hizo zililipwa ili Wasanii watangaze Utalii wa ndani katika Mikoa sita ya Tanzania, lakini Wizara ilishindwa kuhakiki wigo wa huduma iliyotolewa.

Amesema kiasi hicho cha fedha kilicholipwa kwa Wasafi hakiendani na Sheria za matumizi ya fedha za umma.


Habari kubwa kwenye magazeti leo, Aprili 9, 2021
TFF yarudisha kombora kwa Mwakalebela