Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali CAG, Prof.  Mussa Assad amefunguka kufuatia majadaliano yanayoendelea nchini juu ya trilioni 1.5 zinazodaiwa kutooneshwa matumizi yake ametoa msimamo wake juu ya majukumu yake na kudai kwamba hatumii utashi binafsi au kufuata maoni ya mtu yeyote bila kujali nafsi yake.

Amesema ataendelea kutekeleza wajibu wake kwa weledi na kuzingatia sheria za nchi na kuutaka umma utambue kuwa si jukumu lake kuchukua hatua baada ya kuwasilisha ripoti yake kwa mamlaka husika.

Aidha, Chama cha Kijamii cha (CCK), kimesema hakihitaji hesabu za magazijuto katika kukokotoa upotevu wa Trioni 1.5 zilizoibuliwa na Mbunge wa Kigoma, Zitto Kabwe baada ya kuchambua ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali CAG, Prof.  Mussa Assad.

CCK kimeongezea kuwa, CAG amemaliza kazi yake kwa mujibu wa sheria, ni wa wajibu sasa wa bunge kutoa majibu kwa kutumia busara zao ili suala hilo lijibiwe kwa kina na si viongozi wa Serikali kutoa majibu mepesi kama ambavyo yamekuwa yakitolewa toka kuibuliwa kwa swala hilo.

 

Rais wa zamani Malawi kutoka mafichoni, Polisi wammulika
Nyerere ampa ujumbe Rais Magufuli