Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa. Mussa Assad amewaomba radhi wananchi na Serikali juu ya taarifa ya deni la taifa na kusema kuwa yalifanyika makosa ya kimatamshi ya deni hilo.
Profesa Assad ametoa taarifa hiyo mjini Dodoma ambapo amesema kuwa deni halisi ni shilingi trillion 46.08 na ni himilivu hivyo anaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
Katika makabidhiano hayo, yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam, CAG alitahadharisha kwamba deni hilo lililofika Sh46 trilioni kutoka Sh41 trilioni kwa mwaka 2015/2016 sawa na ongezeko la asilimi 12 linatia wasiwasi na Serikali inatakiwa kuchukua hatua kupunguza ukubwa huo.
“Taarifa sahihi kuhusu mwenendo wa deni la Taifa, hadi Juni 30, 2017 lilikuwa Sh46 trilioni. Katika deni hilo, Sh13.34 trilioni sawa na asilimia 29 ni deni la ndani na Sh32.75 trilioni sawa na asilimia 71 la nje. Deni hilo lote ni sawa na asilimia 31 ya Pato la Taifa (GDP) ambalo bado ni himilivu.”amesema leo Prof. Assad