Toleo maalumu la ripoti za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) limedai mikopo kutorejeshwa kwa wakati ndio sababu Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu (HESLB) kushindwa kutoa mikopo yenye thamani ya Trilioni 1.46 kwa wanafunzi wapya na wanaoendelea.

Hii imekuja baada ya serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam( UDSM) kutangaza mgomo kutokana na ugumu wa maisha uliosababishwa  na kutopatiwa mikopo tangu muhula wa masomo uanze.

 Naye mkaguzi wa ofisi ya CAG, Henry Naiman amesema mikopo imeendelea kuwa kikwazo kwa wanufaika, jambo ambalo limepelekea uwezo wa Bodi kutoa mikopo kwa wengine kuwa mdogo

Mbali na UDSM, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), nacho kilitoa wito kwa serikali kuharakisha mikopo

Ambapo CAG Chales Kichere, ametoa wito kwa Bodi ya Mikopo kufanya kazi kwa karibu na Vyanzo au Taasisi nyingine ili kuboresha Kanzi Data yake.

Vanessa mdee aja na 'show' mpya 2020
Bunge la Venezuela kuongozwa na maspika wawili