Klabu ya Newcastle United imekamilisha usajili wa mshambuliaji  Callum Wilson akitokewa Bournemouth kwa ada ya usajili pauni milioni 20 na kusaini mkataba wa miaka minne.

Wilson anaondoka Bournemouth ambapo aliitumikia klabu hiyo katika michezo 184 na kufunga mabao 67.

Hata hivyo haikuwa rahisi kwa Newcastle United kumsajili mchezaji huyo, kutokana na klabu ya Aston Villa kuonyesha nia ya kumuongeza kwenye kikosi chao, lakini dakika za mwisho, alikubaliana na The Magpies.

Wilson anakuwa mchezaji wa 3 kusajiliwa na meneja Steve Bruce katika kikosi chake, akitanguliwa na Jeff Hendrick na Mark Gillespie waliosajiliwa kama wachezaji huru.

 “Baada tu ya kujua Newcastle wamevutiwa na mimi, ilikuwa ni kitu kikubwa sana kwangu. Ni klabu kubwa yenye historia nzuri. Kwa miaka mingi, wamekuwa na washambuliaji wazuri. Kama nitaweza kufikia nusu ya walichokifanya, nitafurahi zaidi.” amesema Wilson.

Kuondoka kwa Wilson inakuwa ni muendelezo ya baadhi ya wachezaji nyota waliotimka kwenye kikosi cha Bournemouth baada ya kushuka daraja.

Tayari Bournemouth imewauza Nathan Ake na Aaron Ramsadale ambao wamesajiliwa na timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya England.

Kubenea mikononi mwa polisi
Balozi wa Iran nchini aagwa