Bingwa namba moja wa Uingereza katika mchezo wa Tenisi, Cameron Norrie ameshinda seti tatu mfululizo dhidi ya Mjapan, Yosuke Watanuki na kusonga mbele katika hatua ya 32 ya mashindano ya Madrid Open.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alitoka akiwa seti nyuma kabla ya kushinda mchezo huo kwa 6-47-6 (7-5).
Watanuki anashikilia nafasi ya 104 akiwa nyuma ya Norrie, lakini alikaribia kumpeleka Muingereza huyo katika seti ya uamuzi katika mashindano hayo ya Hispania.
Mapema juzi Muingereza mwenzake, Dan Evans alitolewa na Mhispania Bernabe Zapata Miralles.
Muingereza namba mbili alijikuta akipoteza kwa 6-3 6-2 kwa bingwa namba 42, ambaye atakabiliwa na Mrusi, Roman Safiullin katika raundi zifuatazo.
Kwingineko, Daniil Medvedev alimfunga Muitalia, Andrea Vavassori kwa 6-4 6-3 na kusonga mbele katika raundi ya 32, wakati Mserbia Dusan Lajovic alipata ushindi mnono dhidi ya bingwa wa dunia namba tisa, Felix Auger-Aliassime, akishinda kwa 6-2 3-6 7-6 (7-5).
Mgiriki Stefanos Tsitsipas alipoteza seti ya kwanza lakini alikuja kumshinda Dominic Thiem, aliyemtoa Muingereza Kyle Edmund na kushinda mchezo wake kwa 3-6 6-1 7-6 (7-5).