Kipindi cha Campus Vibez cha 100.5 Times Fm, kimepanga kuwakutanisha vijana wote hususan wanaochukua masomo ya elimu ya juu na Naibu Waziri wa Ajira na Vijana, Antony Mavunde kesho (Jumamosi) saa mbili kamili asubuhi, katika hotel ya Protea iliyoko Posta jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Ajira na Vijana, Antony Mavunde

Naibu Waziri wa Ajira na Vijana, Antony Mavunde

Tukio hilo muhimu linaloandaliwa na uongozi wa radio hiyo na kuratibiwa na watangazaji wa kipindi hicho, Sadra Temu maarufu kama Sandy B, Raheem Da Prince na DJ One limelenga katika kuwapa fursa vijana kujadili na Naibu Waziri Mavunde kuhusu mbinu za kujikwamua.

Mhariri Mkuu wa Times Fm, Zourha Malisa ameiambia Dar24 kuwa vijana wote wa vyuo vikuu wanakaribishwa kufika katika hotel hiyo mapema saa mbili asubuhi.

“Wote tunatambua kuwa moja kati ya changamoto kubwa zinazowakabili vijana wengi wasomi wanaomaliza elimu ya juu ni ukosefu wa ajira. Na kwakuwa mheshimiwa Mavundo ni Naibu waziri husika na ana uzoefu mkubwa katika nyanja hiyo, tumetengeneza ‘platform’ kwa vijana hao kujadili naye changamoto hiyo kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wakiwa ana kwa ana,” alisema Zoura.

Kipindi cha Campus Vibez ni kipindi cha burudani kinachokuwa hewani usiku wa kila siku za wiki kupitia 100.5 Times Fm kikitoa nafasi kwa vijana kujadili mada mbalimbali huku wakipata burudani kali ya muziki na habari zote kubwa za siku.

Ukweli kuhusu taarifa za ‘El Chapo’ kutoroka tena gerezani wawekwa wazi
BARAZA LA BIASHARA LAANDAA KONGAMANO LA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA INDIA