Kumekuwa na taarifa mbalimbali mitandaoni zikiwahukumu wachezaji wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ kutojua lugha ya kingereza kuwa ndio chanzo kilichopelekea kutofanya vizuri uwanjani, kutokana na kutoelewana na aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mart Nooij.

Julai 2, nahodha wa timu ya taifa, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amelitolea ufafanuzi suala hilo.
“Sisi wachezaji tunaumia zaidi kuliko mashabiki kwa sababu maisha yetu tunategemea mpira tunapopata matokeo mabaya familia zetu zinakaa na njaa, kwanza tunakosa fedha tunazoahidiwa, tunakosa pia kuthaminiwa na watu nje, unajua unapofanya vibaya watu hawawezi kukusapoti, sisi tunaumia zaidi,” alisema.

“Kwa suala la mwalimu kusema kuwa watu hawajui kingereza sio kweli, kwani suala la mpira ni vitendo mwalimu anakuambia fanya hivi hivi na mchezaji unaelewa nini cha kufanya, matokeo yanatokea kwenye mpira unaweza ukashindwa au ukafungwa, sisi tunaumia sana na tunataka matokea mazuri ili tupate kuheshimika kwenye vilabu vyetu”, aliongeza.

Cannavaro ameendelea kutanabaisha kuwa, “tutajitahidi na nitawaambia wenzangu tu ‘force’ (tulazimishe) kila game (mchezo) ambayo itakuwa mbele yetu tuweze kupata matokeo mazuri, sisi kwanza tunatarajia kuanzia mechi na Uganda tukishinda moja tukishinda mbili ilimradi turudishe imani kwa Watanzania”.

Diamond Ampa AY Shukurani Na Heshima Ya Pekee
Mbatia atoa Msimamo Wake Kuhusu UKAWA