Wakati uongozi wa Real Madrid ukijipanga kuimarisha kikosi chake kwa kuwasajili nyota kadhaa hadi sasa akiwemo Edern Hazard, Luka Jovic na kinda Takefusa Kubo ili kuweza kurejea kwenye makali yake kama ilivyo awali lakini baadhi ya wadau wa soka ulimwenguni wameendelea kuukosoa uongozi huo katika maamuzi yake.
Mmoja wa wadau hao ni aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Fabio Capello ameibuka na kusema kwamba miongoni mwa makosa waliyoyafanya Real Madrid ni kumuuza Christiano Ronaldo.
Capello amesema uamuzi wa kumuuza Ronaldo umeigharimu timu hiyo ambapo matokeo yake yalionekana msimu uliopita ambapo Madrid ilimaliza msimu huo pasi na taji lolote tofauti na misimu mitatu nyuma na walitwaa taji la UEFA mara tatu mfululizo na baadhi ya mataji mengine.
Timu hiyo ilimuuza Ronaldo na baadae kwenda kujiunga na Juventus ya Italia ambako huko alifanikiwa kutwaa taji la Ligi hiyo pamoja na kuweka rekodi ya kutwaa mataji ya Ligi kubwa tofauti barani ulaya kwa nyakati tofauti.