Ushindi wa penati tano kwa tatu dhidi ya Rochdale katika mchezo wa mzunguuko wa tatu wa kombe la ligi (Carabao Cup), umeifanya Manchester Utd kupambanishwa na Chelsea kwenye mzunguuko unaofuata.

Mchezo huo uliochezwa usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Old Trafford ulishuhudia Manchester United wakianza kupata bao la kuongoza dakika ya 68 kupitia kwa Greenwood, kabla ya Matheson hajaisawazishia Rochdale dakika 75.

Matokeo hayo yalizifanya timu hizo kupigiana mikwaju ya penati, na ndipo Manchester United walipoibuka kidedea na kusonga mbele.

Mchezo wa mzunguuko wanne, Manchester United watasafiri hadi jijini London kuwakabilia Chelsea, ambao pia walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao saba kwa moja dhidi ya Grimsby Town.

Mchezo mwingine wa kuvutia kwenye mzunguuko wanne wa kombe la ligi utakua kati ya Liverpool dhidi ya Arsenal, ambao utachezwa kwenye uwanja wa Anfield mwezi ujao.

Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Manchester City wamepangiwa kuikabili Southampton kwenye uwanja wa Etihad, huku Aston Villa wakipangwa dhidi ya Wolves.

Michezo mingine ya mzunguuko wanne wa kombe la ligi (Carabao Cup).

Oxford Vs Sunderland

Crawley Town Vs Colchester

Burton Vs Leicester

Everton Vs Watford

Carles Puyol aikataa FC Barcelona
Tunda na Whozu watifuana