Cardi B yuko hatarini kufungwa mwaka mmoja jela kufuatia tuhuma za kuhusika kuwapiga wahudumu wawili wa klabu ya usiku, wiki kadhaa baada ya kuanzisha ugomvi wa ngumi na Nicki Minaj.

Rapa huyo ambaye jana alijisalimisha kwenye kituo cha polisi cha New York, alikamatwa rasmi na kufunguliwa mashtaka ya shambulio la kudhuru mwili pamoja na uzembe.

Cardi B akijisalimisha polisi jana

Imeelezwa kuwa mkali huyo wa ‘I Like It’ alitoa maelekezo kwa wasaidizi wake kuwapiga wahudumu wawili wa klabu hiyo na baadaye yeye pia kushiriki kutembeza kipigo, baada ya kusikia kuwa mmoja kati yao alitoka kimapenzi na mumewe Offset.

“Awe ni mtu maarufu au mtu wa kawaida wa mtaani, anatakiwa kuwajibika kwa vitendo vyake vya kihalifu,” alisema Tacopino ambaye ni mwanasheria wa Jade na Baddie G walioshambuliwa.

Kwa mujibu wa sheria, mbali na kifungo cha mwaka mmoja jela, endapo atakutwa na hatia Cardi anaweza kuwekwa chini ya kipindi cha matazamio na kupata matibabu maalum kwa mwaka mmoja.

Cardi aliingia kwenye klabu hiyo na watu wake kwa lengo la kuangalia ‘show’ ya kundi la Migos.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 3, 2018
Bi Sandra ataja baba wa kijacho chake