Aliyekua beki na nahodha wa mabingwa wa Hispania FC Barcelona Carles Puyol, amekataa nafasi ya kuwa meneja utawala klabu hiyo, baada ya kuondoka kwa Pep Segura, mwezi Julai mwaka huu, kufuatia matatizo ya kifamilia.

Rais wa FC Barcelona Josep Maria Bartomeu amethibitisha alikua na mpango wa kufanya kazi na gwiji huyo kuanzia mwezi huu, lakini alipomfikishia taarifa za uteuzi, alizikataa.

Bartomeu amesema, aliamini Puyol angekua mtu sahihi katika upande wa utawala, kufuatia mchango wake mkubwa aliowahi kuutoa klabuni hapo, akiwa kama mchezaji kuanzia mwaka 1999 hadi 2014.

“Nimefikiria kwa kina kuhusu ofa ya klabu yangu, nimeona si kwa wakati huu, ninamshukuru kila mmoja aliechangia mawazo ya kuniteua,” Ameandika Puyol kwenye ukurasa wake wa Twitter.

“Haikua rahisi kukataa nafasi hiyo, lakini imenilazimu kutokana na sababu mbalimbali, nitaendelea kuiheshimu na kuipenda klabu yangu na ninaamini ipo siku nitarudi kuiongoza kwenye nafasi yoyote.”

Endapo Puyol angekubali kuchukua nafasi ya utawala klabuni hapo, angefanya kazi na rafiki zake Eric Abidal ambaye ni mkurugenzi wa michezo, sambamba na mkurugenzi wa soka la vijana Patrick Kluivert.

Video: Makonda 'Nahujumiwa', Siku 550 za moto wa IGP Sirro
Carabao Cup: Man Utd yapelekwa London, Arsenal yaangukia Anfield