Kiungo anayeelezwa kuwa ni fundi wa kucheza eneo la ukabaji na ushambuliaji, Carlos Stenio Fernandes Guimaraes ‘Carlinhos’, mapema hii leo alijiunga na wachezaji wenzake wa Young Africans mazoezini.

Kiungo huyo kutoka nchini Angola aliwasili nchini jana akitokea kwao, na kupokelewa kwa shangwe na mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati.

Baada ya kufika mazoezini, ‘Carlinhos’ alipokelewa kwa shangwe na wachezaji wenzake, wakiongozwa na mchezaji kutoka DR Congo Mukoko Tonombe.

Hata hivyo Tonombe alimkaribisha maezoezini hapo kwa kumtaka acheze kati kati ya wachezaji wengine wa Young Africans ambao walikua wameweka duara.

‘Carlinhos’ alishindwa kufanya hivyo na ndipo Tonombe alipochukua jukumu la kumuongoza.

Huo umekua kama utamaduni wa wachezaji wa Young Africans katika kipindi hiki tangu, ambapo waliowahi kufanyiwa hivyo ni wachezaji kutoka DR Congo Mukoko Tonombe na Tuisila Kisinda ambao walionyesha shoo ya kibabekati kati ya wachezaji wenzao mazezini hapo.

Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Michael Sarpong naye alikumabana na jambo kama hilo lakini alifanikiwa kuwaburudisha wachezaji wenzake wa Young Africans.

Kikosi cha Young Africans kinaendelea na mazoezi katika viwanja vya chuo cha Sheria jijini Dar es salaam, kwa ajili ya kujiweka FIT kuelekea mpambano wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Eagle Noir ya Burundi.

Mpambano huo utachezwa siku ya Jumapili  Uwanja wa Mkapa jijini Dar es salam katika kilele cha siku ya MWANANCHI.

TCU yafungua dirisha 2020/21
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 26, 2020