Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amekanusha taarifa za kwenda kuitumikia timu ya Taifa ya Brazil msimu ujao kama ambavyo taarifa zilivyowahi kutoka majuma kadhaa nyuma.

Ancelotti amesema hizo ni tetesi tuu yeye anafurahia kuwa Real Madrid.

Malengo yake ya sasa na msimu ujao ni kuwapa mataji Madrid kama ambavyo amekuwa akifanya mara kadhaa.

Don Carlo ambaye anatajwa kuwa ndiye kocha mwenye mafanikio makubwa zaidi duniani, amesema kuinoa timu kama Brazil ni ndoto ya kila kocha, lakini kwake yeye anaona bado kwa sasa.

“Nafikiri hizi ni taarifa kama ambavyo imekuwa kawaida kwa wachezaji na makocha kwenye masoko ya mpira duniani. Nafurahia kuwepo Madrid.

“Nafurahia kufanya kazi kwenye klabu kubwa na yenye mafanikio makubwa duniani. Sijui kuhusu jambo lingine kwa sasa,” amesema.

Ikumbukwe hivi karibuni taarifa zilitoka kuwa Don Ancelotti tayari amesaini mkataba wa kuinoa Brazil na msimů ujao hatokuwa na Madrid.

Wanaojihusisha na siasa badala ya utendaji kufikishwa Ikulu
CBT kuanzisha Shamba darasa la Korosho Kimange Sekondari