Kocha Mkuu wa Real Madrid Carlo Ancelotti amesema kuwa kikosi chake cha Real Madrid tayari kimekamilika hata bila kuongezwa kwa Kylian Mbappé baada ya ushindi wao wa mchezo wa kirafiki wa 2-0 dhidi ya Manchester United kule Houston nchini Marekani, juzi Alhamis (Julai 27).
Jude Bellingham aliyewasili Madrid kwa kitita cha Euro Milioni 103 alifunga bao la kwanza mapema kwenye uwanja wa AT&T, kabla ya mchezaji mwingine aliyesajiliwa majira haya ya joto, Joselu kuongeza la pili.
Ancelotti amekuwa akisema mara kwa mara kwamba anafuraha na kikosi chake, licha ya kuondoka kwa mchezaji namba tisa Karim Benzema na viungo huku Mbappé, aliyezuiwa na Paris Saint-Germain akihusishwa kujiunga na The Galacticos.
“Kikosi kiko sawa. Hatutakuwa na matatizo na kikosi. Kikosi ni kizuri. Kimekamilika.” alisema Ancelotti.
Alipoulizwa kuhusu Mbappé, Kocha huyo kutoka Italia huyo alilikwepa swali ili na kukusitiza kikosi chake kimekamilika na kuomba kuulizwa swali lingine, alijibu; “Swali linalofuata.”
Ushindi huo dhidi ya United unamaanisha kuwa Madrid wameshinda mechi zao zote mbili za kirafiki za kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani hadi sasa, baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya AC Milan kwenye uwanja wa Rose Bowl huko Pasade- na, California.
Miamba hao wa Ligi Kuu ya Hispania, LaLiga, wamewaongeza Bellingham, Joselu, Arda Guler, Fran Garcia na Brahim Diaz kwenye kikosi chao msimu huu wa joto.
“Bao la Bellingham limeonesha ubora alionao. Anazidisha mbio zake kutoka kwa kina kirefu.,” aliongeza Ancelotti.
Antonio Rudiger alimpa pasi nzuri na kufunga. Na la Joselu ni bao ambalo hulioni mara kwa mara.
Mbappé anafanya mazoezi na wachezaji wa akiba wa PSG baada ya kuachwa nje ya ziara yao ya Japan, huku klabu hiyo ya Ufaransa ikitaka kuweka shinikizo kwa fowadi huyo ama kuongeza mkataba wake zaidi ya msimu ujao wa joto, au kuhama sasa, badala ya kuondoka kwa uhamisho wa bure.
Huku Joselu akiwa ndiye fowadi pekee wa asili katika kikosi cha Madrid kwa sasa, Ancelotti amekuwa akijaribu mfumo mpya wa 4-4-2 akiwa na Vinicius Junior na Rodrygo.
“Nadhani Vinicius anabadilika. Anapenda kucheza ndani zaidi kidogo… Rodrygo na Vinicius ni hatari sana wakiwa na mpira. Tunaweza kuwa moja kwa moja katika mabadiliko, na ubora wa Bellingham utasaidia hilo.”
Real Madrid itacheza na FC Barcelona mjini Arlington, Texas baadae leo Jumamosi (Julai 29), na kisha Juventus mjini Orlando, Florida Agosti 2. kabla ya kurejea kutoka Marekani.