Imefahamika kuwa Carlo Ancelotti atakuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Brazil, baada ya kumalizana na Magwiji wa jiji la Madrid-Hispania Real Madrid.

Shirikisho la Soka nchini Brazil limethibitisha taarifa hizo, baada ya kufikia makubaliano ya awali na Kocha huyo kutoka nchini Italia, ambaye ataendelea kuhudumu Real Madrid hadi mwaka 2024.

Ancelotti, mwenye umri wa miaka 64, atakuwa kocha wa timu ya taifa kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya ukocha, akichukua nafasi ya Tite, ambaye aliondoka kwenye nafasi hiyo baada ya kushindwa kufanya vizuri wakati wa Fainali za Kombe la Dunia 2022, ambapo kikosi chake kiliondolewa katika hatua ya Robo Fainali na kwa kufungwa na Croatia.

Kwa sasa, Kocha mkuu wa Fluminense Diniz ndiye Mkuu wa Benchi la Ufundi la Brazil, akichukua mikoba ya Kocha wa Timu ya Taifa ya taifa hilo chini ya Umri wa miaka 20 (U-20) Ramon Menezes, ambaye alipoteza mechi mbili kati ya tatu za kirafiki mapema mwaka huu kama Kocha wa muda wa kikosi cha wakubwa.

Diniz, mwenye umri wa miaka 49, ataendelea na kibarua chake katika klabu ya Fluminense na kujiunga na Brazil kwa mechi za kufuzu Kombe la Dunia pekee.

Baada ya hapo Ancelotti atachukua nafasi kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Amerika ya Kusini ‘Copa America 2024’ na Fainali za Kombe la Dunia 2026.

Kocha huyo ataunganishwa tena na wachezaji ambao tayari amewafundisha, kama vile Vinicius Jr, Neymar Jr, Rodrygo, Eder Militao na wengineo.

Dilunga afunguka kilichomng'oa Simba SC
Leandre Onana apewa maua yake Simba SC