Kocha Mkuu wa Real Madrid Carlo Ancelotti amekanusha kuwa kikosi kudaiwa kutegemea zaidi mabao ya Jude Bellingham baada ya timu hiyo kutoka sare ya bila kufungana na Rayo Vallecano kwenye mchezo wa Ligi Kuu Hispania, La Liga juzi Jumapili (Novemba 05).

Sare ya bila kufungana kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu ilikuwa ni mara ya kwanza msimu huu kwa Madrid kushindwa kufunga na kuwafanya wabaki nafasi ya pili kwenye msimamo, wakiwa na alama mbili nyuma ya vinara Girona.

Bellingham, ambaye amefunga mabao 10 katika mechi 11 za La Liga msimu huu, alicheza dakika zote 90, lakini jana Jumatatu (Novemba 06) alitarajiwa kufanyiwa vipimo baada ya kuanguka vibaya katika kipindi cha kwanza na alihitaji matibabu kwenye bega.

“Bellingham alikuwa na tatizo la bega na atafanyiwa tathmini,” alisema Ancelotti katika mkutano wake na waandishi wa habari baada ya mechi.

“Aliweza kuendelea. Atafanyiwa vipimo, tutegemee si mbaya na anaweza kucheza Jumatano (dhidi ya Braga kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya).”

Ancelotti alisisitiza kwamba Madrid wana wafungaji wa kutosha wa mabao katika kikosi chao kuweza kustahimnili iwapo Belingham hawezi kupata bao, au hayupo.

“Hapana. Tuna rasilimali nyingi.” alisema. “Juzi tumetengeneza nafasi na Valverde, pamoja na Vinicius Junior, Joselu na Rodrygo.”

Madrid walipiga mashuti 22 dhidi ya Rayo, matano yakilenga goli, lakini hawakuweza kupata matokeo.

“Tulijaribu kwa krosi, tulijaribu kupitia mipira, tulijaribu kwenda moja kwa moja, tulijaribu kila njia na haikufanikiwa.” aliongeza Ancelotti.

“Kila mtu anajua inaweza kutokea. Lazima uamini hadi mwisho, na wachezaji walijaribu hadi sekunde ya mwisho.

Gamondi afichua alipoishika Simba SC
Wafugaji wapigwa marufuku kuwapeleka Watoto kuchunga