Beki kutoka nchini Uholanzi Virgil van Dijk huenda hajawa kwenye kiwango bora msimu huu, lakini Jamie Carragher amesema hakuna beki wa kati katika Ligi Kuu ya England ambaye amewahi kuwa na mchango mkubwa kwa timu yao zaidi yake.

Carragher amemtetea Beki huyo kupitia Mtandao wa Kijamii wa Twitter, akipendekeza Van Dijk alikuwa bora zaidi kuliko mlinzi wa zamani wa Manchester United, Nemanja Vidic, na alikuwa amefika kiwango sawa na Kevin De Bruyne katika miaka ya hivi karibuni.

Hilo lilikuja baada ya Liverpool kutoka sare ya mabao 2-2 na Arsenal kwenye Uwanja wa Anfield Jumapili (April 09), wakati safu ya ulinzi ya Jurgen Klopp ilipoonekana kupwaya huku Gabriel Martinelli na Gabriel Jesus wakipachika mabao.

Uchezaji wa Van Dijk umetiliwa shaka mara kwa mara msimu huu, huku Carragher akitoa tathmini kali ya beki huyo baada ya Liverpool kuchapwa mabao 5-2 na Real Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Februari mwaka huu.

Wakati nahodha wa zamani wa Liverpool, Carragher alikiri hali ya kukatisha tamaa ya msimu wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, anaamini hakuna beki wa kati anayekaribiana na Van Dijk katika enzi hii ya Ligi Kuu England.

Carragher aliandika: “VVD (Van Dijk) ni bora zaidi kuliko Vidic.

Kagera yapokea Bilioni 2 ujenzi Kituo magonjwa ya mlipuko
Ahmed Ally: Baleke ametuahidi mazito April 16