Kiungo kutoka nchini Brazil Casemiro anajuta kwa kufanya uamuzi wa kujiunga na Manchester United huku klabu hiyo ikitaka kumsajili kiungo wa Benfica, Joao Neves.
Casemiro alijiunga na United kwa mkataba wa Pauni Milioni 70 msimu uliopita wa kiangazi na kumaliza safari yake ya miaka tisa ya kubeba mataji akiwa na Real Madrid.
Akiwa Hispania alishinda mataji matano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, kwenye safu ya kiungo akiwa pamoja na Toni Kroos na Luka Modric, ambapo watatu hao waliunda ushirikiano wa kutisha ambao kwa kiasi kikubwa.
Kuwasili kwa Mbrazili huyo United mwanzo kulisaidia kubadilisha timu ya Erik ten Hag katika msimu wake wa kwanza, na kuongeza usawa, udhibiti kwenye eneo la kiungo.
United walimaliza ukame wao wa miaka sita wa kutotwaa taji, na kisha wakabeba Kombe la Ligi ‘Carabao Cup’, huku pia ikifika fainali ya Kombe la FA na kumaliza katika nafasi tatu za juu ligi.
Hata hivyo kiwango cha Casemiro kimedorora msimu huu na maswali yameibuka juu ya nafasi yake kwenye kikosi.
Sofyan Amrabat na Mason Mount wote walijiunga msimu huu wa joto ili kuongeza ushindani kwa nafasi ya kiungo.
Ripoti kutoka El Nacional sasa inaeleza jinsi Mbrazil huyo, ambaye ana mkataba wa muda mrefu United, sasa anajutia kubadilika kwa maisha yake kutoka Madrid mwaka mmoja uliopita.