Msimu mpya wa tamasha la Castle Lite Unlocks umetangazwa rasmi ambapo milango ya kununua tiketi kwa bei ya promosheni ni Februari 20, 2020 huku msanii mkubwa wa Hip Hop barani Afrika akitarajiwa kulipamba tamasha hilo.

Kwa mujibu wa Castle Lite, chapa ya bia inayotajwa kuwa bia bora zaidi Afrika, tamasha hilo linalotambulika zaidi kama kinara wa kusukuma harakati za Hip Hop barani Afrika, Februari 20 itauza teketi hizo kwa bei ya Randi ya Afrika Kusini 50 (R50) ambayo ni sawa na Shilingi 8,000/= za Kitanzania na itakuwa ikiongezeka kwa kiasi cha R50 kila baada ya nusu saa. Hivyo, kwa watakaowahi kununua watafaidi burudani hiyo ya kipekee na ya kimataifa kwa gharama ndogo zaidi. Hivyo, unavyozidi kuchelewa kukata tiketi yako ndivyo bei yake inavyozidi kuongezeka.

Wameongeza kuwa mashabiki wakubwa wa harakati za Castle Lite Unlocks watalazimika kununua tiketi hizi za Mapema kabla ya kufahamu ni msanii gani mkubwa ataongoza tamasha la mwaka huu.

Castle Lite wameeleza kuwa mpangilio huu wa bei inayobadilika unawawezesha kupata fursa ya kipekee ya kushiriki tamasha la Unlocks kwa kulipia tu sehemu ndogo ya gharama huku wakiweka imani yao katika uwezo wa waandaaji wa tamasha kuleta nyota wakubwa duniani na Afrika Kusini.

“Ikiwa bado unajiuliza ni nyota gani wakubwa watashiriki 2020, utahitajika kusubiri kwa siku chache tu. Jambo pekee ambalo chapa yetu inaweza kusema kwa sasa ni kwamba, msanii mashuhuri mwenye tuzo kede kede na aliyewahi kuvunja rekodi kadhaa, mwenye mashabiki duniani kote sio tu ataleta kipaji chake cha kipekee Mzansi, lakini pia kutakuwa na mabadiliko makubwa katika namna Castle Lite inavyofanya mambo kulinganisha na kipindi cha nyuma,” imeeleza taarifa ya waandaaji wa tamasha hilo.

Wamewahimiza wapenzi wa burudani kuhakikisha wanajinyakulia tiketi mapema kupitia www.castlelite.co.za Alhamisi, 20 Februari kuanzia R50 saa 15:00. Baada ya hapo tiketi zitaongezeka kwa R50 kila baada ya dakika 30 mpaka saa 19:30 ambapo watamtangaza rasmi msanii wa kimataifa. Baada ya hapo, mashabiki watanunua tiketi za tamasha la Castle Lite Unlocks kwa bei ya kawaida.

“Castle Lite Unlocks iko mwaka wake wa 10 sasa na imekuwa ni miaka 10 ya vipaji vya muziki vya kipekee, kusherehekea tamaduni ambayo imeiteka dunia na kusogeza sanaa ya Hip-Hop ya Afrika mbele. Sasa ni muda wa kupiga hatua na kuipeleka Unlocks katika ngazi nyingine huku tukirejesha heshima kwa tamaduni ya Hip-Hop ndani ya Afrika,” Mkurugenzi wa Chapa ya Castle Lite, Silke Bucker amewaambia waandishi wa habari.

“Na ni njia gani bora ya kuingia katika muongo unaofuata wa Unlocks zaidi ya kutoa fursa kwa wateja wetu kuwa wa kwanza kununua tiketi kwa bei ya kutupwa katika tamasha kubwa la Hip-Hop barani Afrika, likiongozwa na wasanii wa kimataifa wanaowapenda,” aliongeza.

Kwa taarifa zaidi tembelea www.castlelite.co.za au fuata kurasa rasmi katika mitandao ya kijamii, na wafuate kupitia Facebook: Castle Lite |Twitter: @CastleLiteSA | Instagram: @CastleLiteSA | #CastleLiteUnlocks

Rapa 50 Cent amkana French Montana

Dkt. Mashinji ahamia CCM, ataja kilichomkimbiza Chadema
Mwiko wanufaika wa Tasaf kuchangia miradi ya maendeleo