Kiongozi wa Catalonia Carles Puigdemont amesema kuwa Catalonia itatangaza uhuru wake kutoka Hispania siku chache zinazokuja.

Umati wa watu umekuwa ukiandamana Barcelona kulalamikia hatua ya serikali ya kutumia nguvu kuwazuia watu kupiga kura ya maoni ya kudai uhuru wa jimbo la Catalonia, ghasia za polisi wa Uhispania wakati wa upigaji wa kura zilisababisha watu takriban 900 kujeruhiwa.

Haya ni maandamano makubwa kuwahi kutokea katika jimbo la Catalonia na pia Barcelona kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka mingi na Mfalme wa Hispania Felipe VI amesema kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria katika maandalizi ya kupiga kura ya maoni.

Mfalme huyo amesema kuwa hali ya sasa nchini Uhispania sio nzuri na kutaka kuwepo umoja. Wakati wa upigaji wa kura takribani polisi 33 pia walijeruhiwa.

Ni kwa muda mrefu jimbo la Catalonia limekuwa likitaka kujitenga na Hispania na sasainawezekana jambo hilo likatokea kwani watu wacatalonia wanaonekana kupigania jambo hilo kwa vitendo sasa.

Kwa muda wote wa ghasia hizo mashule na sehemu nyingi za huduma zimekuwa zimefungwa huku pia klabu ya Barcelona ikiwa imefungwa.

 

 

Video: JPM atema nyongo, Takukuru wafunguka sakata la rushwa Arusha
Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 4, 2017