Vigogo wa Manchester United, wameripotiwa kuanza mazungumzo ya  kumshawishi mshambuliaji wao kutoka nchini Uruguay Edinson Cavani  ili kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Mazungumzo na mshambuliaji huyo wazamani waklabu ya SSC Lazio ya Italia na PSG ya Ufaransa yanadaiwa kuongozwa na Mkurugenzi mpya wa michezo wa mashetani hao wekundu wa Old Trafford, John Murtough na makamu mwenyekiti mtendaji, Ed Woodward.

Inasemekana kuwa Cavani alichukizwa na namna ambavyo chama cha mpira wa miguu nchini humo kilivyomchukulia hatua za kinidhamu baada ya kuposti maneno yaliyotafsiriwa kuwa ya kibaguzi ilihali halikuwa lengo lake.

Siku chache zilizopita, kocha msaidizi wa timu yake ya taifa la Uruguay, Mario Rebollo alisema kuwa Canavi yupo mbioni kusepa Manchester United kwa lengo la kwenda kutafuta changamoto mpya za soka sehemu nyingine.

Serikali yadhamiria makusanyo makubwa, "Tumieni akili zaidi kuliko nguvu"
Sarpong: Ninapenda kufunga